Mbunge wa Kyela na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amesema kuwa mashtaka mbalimbali yanayoletwa hivi sasa dhidi ya watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi bado ni "mepesi" na anatajia kuwa baada ya uchunguzi kufanyika zaidi mashtaka hayo yatabadilishwa na kuwa mazito yakiwemo yale ya sheria ya Uhujumu uchumi.
Hayo na mengine mengi ameyasema katika mahojiano yake na KLHN ya mwanakijiji.com ambayo yalirushwa moja kwa moja siku ya Jumapili. Unaweza kuyasikiliza mahojiano yote tena kwa kutembelea kwa kubonyeza kiungio hapa chini.
Wakati huo huo ofisi ya Waziri Mkuu imetoa ufafanuzi juu ya kauli za Waziri Mkuu alizozitoa hivi karibuni huko kanda ya ziwa ambapo ilidaiwa alisema mambo ambayo yanayoonekana kutia shime watu kujichukulia sheria mkononi. Unaweza kusoma majibu hayo na maswali ambayo tuliyatuma kwao mahali pekee kwenye http://www.mwanakijiji.com
Licha ya majibu hayo msimamo wangu ulioko kwenye kijarida cha "Cheche za Fikra" na mapendekezo ninayoyatoa kwenye gazeti la Tanzania Daima la leo bado yanasimama.
Unaweza kupata nakala yako ya "Cheche za Fikra" kwa kumuandikia Mhariri wetu kwa anuani ya mhariri@klhnews.com au kwa kujiandikisha kwenye http://www.mwanakijiji.com ambapo utaweza kupata nakala hiyo bure.
Usikose mahojiano yetu na Dr. Harrison Mwakyembe ambayo yatarushwa siku ya Jumatano.
Kesho siku ya Jumapili kuanzia majira ya saa saba za mchana (EST) sawa na saa tatu za usiku (Saa za Afrika ya Mashariki) tunatarajia kuwa na mahojiano na Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kampuni ya Richmond.
Ni matokeo ya Kamati hiyo ndiyo yaliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Edward Lowassa kujiuzulu na hatimaye Baraza la Mawaziri kuvunjika. Tutatungumza na Dr. Mwakyembe karibu mwaka mmoja kamili tangu matukio yale ya Februari 2008, matukio ambayo yalikuwa ni ya kihistoria. Tutazungumza naye pia mambo mengine ya kitaifa saa na wakati huu ambapo Taifa letu linapitia katika mabadiliko makubwa ya kifikra.
Utaweza kusikiliza mahojitano yetu kupitia tovuti yako hii "live" kwenye http://www.mwanakijiji.com
Siku chache zijazo Shirika letu la ndege linaloongozwa na Bw. David Mattaka linatarajiwa kupewa mabilioni mengine ya fedha za walipa kodi wa Tanzania ili liweze kurusha ndege zake katika kuitikia wito wa Rais Kikwete kuwa ndege hizo zirudi angani mapema iwezekanavyo.
Pamoja na matatizo makubwa ya kiutendaji, maono, na usimamizi uliosababisha shirika hilo kuingia katika mikataba kama ya majaribio serikali imeonelea ni bora kutoa fedha zaidi ili ndege za ATCL litanue mbawa zake angani.
Katika toleo letu la Cheche wiki hii tunachambua wazi ni kwanini tunaamini kuwa kuipatia fedha zaidi na kwa haraka bila ya kufanya mabadiliko ya mfumo, muundo, utendaji na maono ya shirika ni sawa kabisa na kujaribu kujaza pipa lililotoboka na kwa haraka kukimbia tena kisimani kuchota maji mengine!
Kama serikali ya CCM inaamini kuwa tatizo la ATCL ni fedha tu na hivyo kuwapa fedha kutatatua matatizo mengine basi tunapendekeza serikali itoe bilioni 400 na kuwapa ATCL chini ya uongozi huu huu na wenye mipango ile ile ya utendaji. Kama Serikali ya CCM inaamini kuwa kwa kufanya hivyo itatatua tatizo la huduma za ATCL basi ifanye hivyo mara moja ili hatimaye matatizo yote ya ATCL yatoweke kama ukungu wa alfajiri na yapotelee mbali kama njozi ya Alinacha!
Pata nakala ya "Cheche za Fikra" hapa:http://www.forums.mwanakijiji.com/forumdisplay.php?f=62
M.M. MwanaKJJ
Nikiri ya kwamba nimesikitishwa na kushangazwa sana na baadhi ya ukosoaji wa Mhe. Simba kufuatia mahojiano yangu naye siku chache zilizopita. Kilichonisikitisha zaidi ni jinsi gani baadhi yetu tuna angalia vitu ambavyo si vya msingi na kuviacha vya msingi; kilichonishangaza zaidi ni jinsi gani wengine wamekuwa wa kali kiasi cha wao wenyewe kuwa kile wanachomtuhumu Mhe. Simba.. arrogance!
Katika mahojiano yangu na watu mbalimbali (kama Dr. Migiro, Dr. Salim, na wengineo) sijawahi kujaribu kumtetea mtu yeyote kwa majibu yake. Hata hivyo katika hili la Mhe. Simba nimeona kilele cha kebehi na kina cha parapanda ya unafiki wa uongo. Wengi wamemhukumu Mhe. Sofia kwa ukali ambao haukustahili na umeenda zaidi ya ukosoaji wa kumjenga mtu!
Mojawapo ya chaguzi ambazo zimekuwa na mvuto wa muda mrefu ndani ya CCM ni ule uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (T) alipatikana.
Mshindi huyo si mwingine bali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Sofia Simba. Safari ya ushindi wake ilikuwa ni safari ambayo wachache wako tayari kuipitia. Ilikuwa ni safari ambayo unapofika mwisho inabidi ujiuliza ulianzaje safari hiyo.
Hivyo KLHN ilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu kuhusu ushindi wake huo na hasa kutupa mwanga kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea kati yake na mpinzani wake katika uchaguzi Mhe. Janeti Kahama.
Pamoja na hayo tumemuuliza maswali ya kutaka kujua kama kweli Rais Kikwete ndiye aliyemtaka agombee na kama ni kweli hotuba ya Rais Kikwete kwenye ufunguzi wa uchaguzi ilikuwa ni ya kumpa mkono wa baraka ili achaguliwe. Pamoja na hayo tulitaka kujua zaidi kuhusu UWCCM utakuwaje chini ya uongozi wake?
Sikiliza mahojiano hayo ambayo yanapatikana kwenye http://www.mwanakijiji.com Kwa maoni au mawazo tuandikie mhariri@klhnews.com
Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Sofia Simba kufuatia ushindi wake siku ya Ijumaa ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wanawake wa CCM (T) Ngazi ya Taifa. Hiyo ndiyo habari inayopamba toleo hili na habari nyingine kem kem. Usisite kuendelea kuwakaribisha watu wengi zaidi kujiandikisha kupata nakala ya kijarida chenu hiki bure kabisa kikiwa na habari ambazo huwezi kuzipata kwa uchambuzi na kina cha kijarida hiki. Lengo letu ni kuwa inapokuja suala la habari za Tanzania, sisi tunataka kuweka kiwango!
Ombi la wiki hii ni kuwa kama uko Tanzania tunakusihi uchape angalau nakala moja na umpatie mtu ambaye hana nafasi ya kupata mtandao!
Mwishoni mwa mwaka jana nilipata nafasi ya kuzungumza na Bongoradio.com kuhusu masuala mbalimbali ya kufunga mwaka. Ninawaletea sehemu kidogo ya mahojiano hayo pamoja na mahojiano niliyoyafanya na Mhe. Dr. Wilbroad Slaa (Karatu-Chadema) kuhusu kilichosababisha mgombea wao msomi mwanasheria Bw. Sambwee Shitambala kushindwa kufuata taratibu rahisi za kuapa kabla ya kushirki uchaguzi huo mdogo.
Baada ya kusikiliza mahojiano hayo piga kura na upande wa kulia wa tovuti hii na utoe maoni yako ni nini unafikiri kilitokea Mbeya Vijijini. Unaweza kusikiliza mahojiano kwa kuingia kwenye "Podcasts" kwa kubonyeza herufi ya "M - Podcast" upande wa kulia wa ukurasa wa mbele wa tovuti yetu Kisha angalia miaka na tarehe ya onesho.
Kwa mawasiliano mengine yote tuandikie mwanakijiji@mwanakijiji.com na kwa kutaka kujiandikisha kijarida cha bure cha "Cheche za Fikra" tuandikie mhariri@klhnews.com
Salaam za mwaka mpya kwako na kwa vyote vilivyo vyako. Kama tulivyoahidi wiki hii inayokuja tutawatumia barua ya taarifa ya mambo tuliyoyafanya mwaka jana na mipango yetu kwa mwaka mpya. Tarajia barua yetu kabla ya toleo lijalo.
Katika toleo hili habari kuu ambayo utaisoma kwenye "Cheche za Fikra" peke yake (Huwezi kuipata kwenye gazeti jingine lolote) ni juu ya timu-kazi ya maafisa wa Usalama wa Taifa ambao wametawanyika sehemu mbalimbali nchini kufuatilia mauaji ya Albino ili kuweza hatimaye kuyakomesha mwaka huu. Pia habari nyingine motomoto zimo humu na maoni yenye nguvu ya watu mbalimbali kutoka kwenye mtandao.
Tafadhali endelea kuwapatia watu wengine kijarida na waalike watuandikie kwenye mhariri@klhnews.com ili waweze kujipatia nakala zao kwa barua pepe. Tunataka ifikapo Juni, tuwe na wasomaji wanaopata kwa email wapatao 1000! (hadi sasa tunao 168) ukiondoa wanaosoma kwenye mitandao mingine au kudownload toka mwanakijiji.com Hilo halitawezekana isipokuwa kwa ushirikiano wako. Tunataka kuhakikisha moto wa fikra za mabadiliko unazidi kukolezwa taratibu kutoka Mtanzania mmoja hadi mwingine kwa kuwasha "cheche za fikra" mioyoni mwao.
Mabadiliko tuyatakayo, ni sisi wenyewe!
Twende na tuwe Cheche!
The most prominent, provocative, and premier Swahili podcast by an author and political analyst M. M. Mwanakijiji and the crew. The podcast is intended to be an instrument that facilitate positive attitudinal and mentality change among Tanzanians as they try to build a modern, vibrant, and prosperous African nation. This podcast is full of political, socio-economic opinions, news, and commentaries. The show also showcase now and then some Tanzanian music and other talents. To keep yourself in the "loop" of what is going on in Tanzania, you should subscribe to this, it'll be one of the best decisions you have made. If you find this podcast to be interesting, why don't you recommend it to other Tanzanians? It is our mission to reach as many Tanzanians as possible, alone the task will be difficult with your help however, the sky is the limit!