Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_2105143

Sijui kama kweli tunataka mabadiliko au tunaombea mabadiliko yatokee. Sijui kama tunafanya ili kusababisha mabadiliko au tunasubiri wengine wafanye ili tufurahie mabadiliko; Sijui hata kama tunajua vizuri ni mabadiliko gani hasa tunayataka na kama tunataka ni juhudi gani tumezifanya kushiriki kwenye mchakato wa kuleta mabadiliko hayo.

Tunaweza kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kujaribu kubadilishana mawazo mchana kutwa na usiku kucha lakini mabadiliko hayaji kwa kusema. Mabadiliko hayaji kwa kupigiwa magoti au kwa kukemea giza usiku. Mabadiliko husababishwa na kutekelezwa.

Tukijifunza kwenye kampeni ya Obama utaona kuwa Wamarekani hawakuombea tu kuwa kiongozi mzuri au wamtakaye aje na alipojitokeza hawakukaa pembeni kuombea kuwa afanye vizuri ili hatimaye "alete mabadiliko" wanayoyataka. Wamarekani walishirikishwa katika kampeni kuanzia kuchangia fedha, muda wao, vipaji vyao n.k

Je kwanini tunafikiri sisi Tanzania tutapata mabadiliko kwa kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kuoneshana nani anajua nini na anahusika na nini? Mabadiliko ndugu zangu hayaji kwa kunuia au kuwa "kusudio zuri" au kwa kujua ufisadi ulivyo mbaya na fisadi ni nani!!

Mabadiliko huletwa na watu waliokusudia kuleta mabadiliko hayo. Nisikilize.

[PLAY]
460>_2029110
Unaweza kupata sneak ripoti hiyo kwenye http://www.mwanakijiji.com

Password ya kufungulia Ripoti Sneek Pek: meremeta1997

Inapatikana hivi: (Tafadhali angalia masahihisho kutoka taarifa yetu ya Ijumaa) Ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:

* Kupitia Mtandao wa http://www.mwanakijiji.com kuna kitufye cha kuchangia upande wa kulia juu(Donate Button) cha Paypal Inc., Hapo tunaweza kupokea malipo ya kadi za kibenki katika njia ya usalama wa hali ya juu na wachangiaji wote wanamakia sirini (rekodi yetu ya miaka mitatu hatujawahi kuvujisha jina la mchangiaji yeyote yule!).Kadi za Visa, MasterCard, Express zinapokelewa.

* Kwa taasisi au watumishi wa umma (VIPs) ambao kwa sababu za wazi wangependa kutojulikana wasiliana nami kwa email au Private Message na utapata maelezo ya kuwasiliana na Mwandishi wa Habari Mchunguzi wa gazeti la kiingereza la kila siku la nchini aliyepo Tanzania ambaye atapokea fedha hiyo pamoja na email yako ambayo tutakutumia nakala hiyo katika usiri mkubwa. Yeye pia anaweza kupokea kwa njia ya Western Union kwa wale ambao wangependa kutumia njia hiyo.

* Kwa mtu mwingine yeyote tuma fedha kwa njia yarecharge vouchers kwenda namba: 0713444649. Vouchers ziwe ni za tiGO, Zain au Zantel.

Kama mipango yote itakwenda ilivyo, basi tunatarajia kutuma nakala hizo 100 siku ya Jumatano wiki ijayo kwa wale waliochangia. Hivyo ina maana watu wana siku tano za kukamilisha oda zao. Pamoja na ripoti hiyo, tumeambatanisha pia ripoti yetu ya 2006 juu ya “Tracing Reports of Tanzania’s role in arms trafficking”.

Oda nakala yako mapema kwani tutafanya kwa mtindo wa “aliyewahi mpe” – first come, first serve.

NB: - Email moja kwa nakala moja. - Hakuna nakala itakayotangulia mchango; na hakuna mtu atakayepata nakala kabla ya watu wengine. Watu wote watakaokuwa wamechangia watapata nakala zao Jumatano. NO EXCEPTION.

[PLAY]
460>_2024834

Ripoti ya kijarida cha Cheche za Fikra juu ya Meremeta imekamilika. Ina kurasa karibu 50 ikiambatanishwa na vielelezo lukuki ambavyo kwa wengi itakuwa ni mara ya kwanza kuviona hadharani, vielelezo ambavyo serikali yetu na baadhi ya wanasiasa mafisadi imefanya jitihada kubwa kuhakikisha havioni nuru ya siku kwa muda mrefu.

Ndani ya ripoti hii maswali kadhaa yanajibiwa kwa kina (mengine kwa kupita tu). Yanajibiwa si kwa ufundi wa hoja na uzuri wa ushawishi wa maneno bali kwa ushahidi mzito na vielelezo ambavyo vyenyewe peke yake vinatosha kabisa kufunga mjadala huu.

Tunaamini kuwa kama sisi Watanzania hatutasimama na kupinga mambo ya uovu yanayofanywa kwa jina letu basi watawala wetu wataendelea kufanya maovu kwa jina letu. Tunafuata mfano wa Wamarekani waliofichua na kukasirishwa na Ab Ghraib au Waisraeli waliojitokeza kupinga vitendo vya jeshi lao dhidi ya Wapalestina. Tunaamini kwenye uovu, hakuna uzalendo wala undugu – there is no patriotism in the presence of evil!

Baadhi ya Maswali yanayojibiwa:

* Meremeta ilianzishwa kwa ajili ya shughuli gani hasa? * Ni kampuni gani iliingia mkataba na serikali kuunda Meremeta ile August 17, 1997? Ukijibu Triennex basi huna budi kuipata ripoti hii kwani utakuwa umekosea. * Je Tanzania inahusika vipi katika usafirishaji wa silaha haramu katika eneo la maziwa mazuu na ni kina nani wanahusika (majina yanatajwa!). * Je yule Mfanyabiashara ya Kifo Victor Bout amewahi kutumia Tanzania kama njia ya kusafirisha silaha haramu kwenda kwenye nchi zenye machafuko? Angalia picha uamue mwenyewe! Vipi kuhusu Dr. K.M? * Kwanini Meremeta ilianzishwa 1997 na si mwaka mwingine wowote? * Unamkumbuka mzee wa “Vijisenti”? Kwanini tunaamini SFO walikosea kuhusisha fedha za Chenge na Rada. * Kwanini Waziri Mkuu mmoja wa zamani aliita mambo ya Meremeta ni ya “Aibu” na kujulikana kwake “kungesababisha wafadhili watunyime misaada”? * Barua ya CCTI kuelekea The Hague, EU, US na taasisi za kimataifa za haki za binadamu. * N.k!!

Excerpts:

Quote: Kwamba Meremeta ilikuwa kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo halikuwa na utata. Aliyekuwa Rais wa Tanzania Bw. Benjamin Mkapa akizungumza wakati akifungua Bunge la Muungano Novemba 20, 2000 alisema wazi kuwa atatilia mkazo kuhakikisha kuwa kampuni ya Meremeta inaendelea kusaidia wachimbaji wadogo wadogo. Hata yeye hakuihusisha Meremeta na siri za usalama wa taifa au na kiwanda cha Nyumbu...

Quote: Kampuni ya Vickers OMC ya Afrika Kusini ilibadilishwa baadaye na kununuliwa na kampuni ya BAE Sysytems ya Uingereza na kugeuzwa kuwa BAE Land Systems ambayo inahusika na utengenezaji wa magari ya kijeshi na hasa yale yenye kukabiriana na mazingira magumu. Hivyo ushirikiano wa TATC na Vickers OMC una mantiki. Na kwa kadiri ya kwamba ulitangazwa Bungeni tunajua kuwa haukuwa siri....

Quote: Kuhusu uamuzi wa kusitisha shughuli za Meremeta jambo la msingi hapa lijulikane ni kuwa si kwa sababu ya matatizo ya bei ya dhahabu au uzalishaji mdogo. Kuifunga Meremeta kulitokana na matatizo ya fedha ambayo yalikuwa yanaikabili kampuni ya Triennex na kampuni mama yake..

Quote: Miongoni mwa vikosi ambavyo Mandela na wenzake walitaka vivunjwe kabla ya wao kuachiliwa ni 32 Battalion, Koevoet, na vile vya Kipelelezi (reconnaissance units). Mojawapo ya vikosi hivyo ni kile cha (censored)[1] ambacho kilikuwa ni kikosi cha kijasusi ambacho kilikuwa kinahusika na mauaji na mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya watu mbalimbali waliokuwa wanatishia utawala wa Kikaburu...

[1] Tume ya Ukweli na Upatanisho, Juzuu ya 2, 2003 Uk. 39

Inapatikana hivi: Ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:

* Kupitia Mtandao wa http://www.mwanakijiji.podomatic.com kuna kitufye cha kuchangia upande wa kulia (Donate Button) cha Paypal Inc., kwenye ukurasa wa mbele (homepage - siyo ukurasa wa forum). Hapo tunaweza kupokea malipo ya kadi za kibenki katika njia ya usalama wa hali ya juu na wachangiaji wote wanamakia sirini (rekodi yetu ya miaka mitatu hatujawahi kuvujisha jina la mchangiaji yeyote yule!).Kadi za Visa, MasterCard, Express zinapokelewa.

* Kwa taasisi au watumishi wa umma (VIPs) ambao kwa sababu za wazi wangependa kutojulikana wasiliana nami kwa email au Private Message na utapata maelezo ya kuwasiliana na Mwandishi wa Habari Mchunguzi wa gazeti la kiingereza la kila siku la nchini aliyepo Tanzania ambaye atapokea fedha hiyo pamoja na email yako ambayo tutakutumia nakala hiyo katika usiri mkubwa. Yeye pia anaweza kupokea kwa njia ya Western Union kwa wale ambao wangependa kutumia njia hiyo.

* Kwa mtu mwingine yeyote tuma fedha kwa njia yarecharge vouchers kwenda namba: 0713444649. Vouchers ziwe ni za tiGO, Zain au Zantel.

Kama mipango yote itakwenda ilivyo, basi tunatarajia kutuma nakala hizo 100 siku ya Jumatano wiki ijayo kwa wale waliochangia. Hivyo ina maana watu wana siku tano za kukamilisha oda zao. Pamoja na ripoti hiyo, tumeambatanisha pia ripoti yetu ya 2006 juu ya “Tracing Reports of Tanzania’s role in arms trafficking”.

460>_1997741

Hi everyone; I'm back, wounded and limping but still kicking LOL. With some of my "little ones" we were able to travel extensively through Europe, US and Costa Rica as well as making some contacts in Singapore, U.A.E (this was published in one of previous Cheche editions. What we have discovered is nothing less than shocking!

I visited the so called Headquarters of Dowans S.A in Costa Rica and had access to relevant organs that deal with businesses there. Some of the things we were able to raise with the Costa Rican gvt and the US gvt were addressed in the meeting in London when the major economic powers addressed the current economic crisis. If you can recall, Costa Rica was named as one of the countries that unless they change their legal framework concerning offshore accounts they will be blacklisted. We are glad as we left the Costa Rican gvt decided to change some of the laws and regulations. We are eternally grateful to those people who made the trip worthy taking and fruitful.

We learned a number of things about Dowans:

a. If It was registered in Costa Rica then simply as a briefcase company. Due to the legal and procedural laxity that existed then in Costa Rica it was very easy for some shady businessmen to appoint a "lawyer" who would act as their middleman and a point of contacts.

After our extensive investigations through different lawyers organisations we were unable to find the lawyer involved with Dowans nor his/her address or whereabout. One authority told us confidently that such a person does not exist except in papers.

b. We visited the offices of Dowans Costa Rica as indicated in their BRELA forms. In these forms Dowans (T) has listed two companies as one of the major shareholders, one is Dowans S.A of AVENIDA DE LA ROSAS 3J CALLE BLANCOS, 1150 sAN JOSE, COSTA RICA and the other company is a major Singaporean company and world world leader in Port Management.. Portek Internation of 20 HARBOUR DRIVE #02-01 PSA VISTA, SINGAPORE 117 612 (Portek International Limited).

The later (Portek) assured us with no qualifications that it has no share, none whatsoever in the Dowans (T). And it is not involved in energy products in Tanzania. The only project they had was the sale of some logistics equipments to TICTIS. This can be verified easily by contacting: Tel: (65) - 6873 1114 or Fax: (65) - 6873 2224

The former (Dowans S.A) has been a pain in some places better left unmentioned. The report of our investigation team under my able leadership came to this conclusion "there is no such a business in Costa Rica operating under that name".

Indeed my visit to the address mentioned in BRELA forms led me to a free trade zone. A check of the business located there revealed no such company. After combing public and private records such as the National Registry of Costa Rica, Telephone, electricity, automobiles and database searches all revealed nothing. Not about Bernal Zamora Alce (the "lawyer") nor the company itself.

Our conclusions then are as follows:

a. Dowans entered into Tanzania under false pretenses, providing misleading information and therefore has engaged in fraud.

b. Due that fact in a, Dowans in Tanzania was wrongly registered and its activity as a company had no legal basis

c. Due to (a and b) Dowans lacks legal standing in our courts to ask compensation as an illegal entity operating illegally.

d. The government should seize all of Dowans assets and take everybody who was involved in enabling this company to enter into a contract with Tanesco to a court of law for abusing their offices and authority.

e. Its choice of Costa Rica as a country of incoporation (knowing fully the laxity and the nature of their tax laws and their business regime) was done with the full blessings of two longtime friends. One is the legal director of Dowans Tanzania Gen (rtd) Mohammed Al-Adawi and the other a prominent businessman and politician.

We have finished the incredible work on Meremeta going back to the time of Wemba Dia Wemba and the second Congo War. We have submitted our work to our commander of ideological battles to decide if he would publish them or due to the explosive nature (no pun intended) of the allegations he would not publish in Cheche.

After we have bankrupted him he wants to charge a one time 25USD for the Special Edition of Cheche on Meremeta (good luck M!).

It is the choice for the CCM MPs to continue to support their corrupt government or to take it to task and restore the rule of law. We hope a courageous CCM MP will bring the issue of Dowans to the floor of the National Assembly and call for an independent inquiry to refute the allegations we have raised or confirm them. We believe such an inquiry will have more resources to dig more and do more than we did with our very limited budget. We have done our part.

Thanks M for giving us another mission. We are ready to fly again.

Note: Kwa wale walioko nje ya nchi wataweza kupata kijarida hicho Maalum (kwa kweli ni Ripoti zaidi kuhusu Meremeta kuliko kijarida ulichokizoea) kwa kununua aidha kwa kutumia credit cards au paypal TU. Kwa walioko Tanzania na ambao wangependa kutumia fedha taslimu au Western Union wasiliana nami kwa email hii ili tuweze tuweze kukupatia taratibu zitakavyokuwa. Kama uko nje ya nchi na hauna credit/debt card au paypal na ungependa kukipata njia itakuwa ni hiyo ya Western Union kwenda Tanzania japo ukilinganisha bei na gharama inaweza kuwa siyo mpangilio mzuri. Mhariri Mtendaji M.M.
[PLAY]
460>_1958996

Kwamba Rais mstaafu Mkapa alitumia madaraka yake vibaya alipojipatia yeye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona Mgodi wa Kiwira halina shaka. Kwamba katika kufanya hivyo alivunja Katiba na alipaswa kuondolewa madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46 ya Katiba kwa kuvunja vipengele kadhaa vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya 1995 na mabadiliko yake nalo halina shaka.

Chenye kuleta tatizo ni jaribio la serikali ya sasa kufanya makosa aliyoyafanya Mkapa akiwa madarakni kuwa ni kama "bahati mbaya" au "kupitiwa". Tatizo wanalolileta ni kuwa sheria haipaswi kufuatwa na watu wote na mtu ambaye ni Rais basi anaweza kufanya lolote atakalo akijua kuwa atatetewa.

Uamuzi wa kurudisha Kiwira mikononi mwa serikali ni ushahidi wa wazi kuwa Mkapa alifanya makosa ambayo kimsingi ukiunganisha na mambo mengine yalikuwa ni ya uvunjaji wa sheria na kwa hakika yangempasa afikishwe mahakamani kujibu mashtaka mazito dhidi yake.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Pinda anasema mataifa ya nje yanamtambua na kumpenda Mkapa kwa kuwa ni mtu mwadilifu. Na zaidi ameliambia taifa kuwa anaamini kuwa Mkapa si "fisadi" kwa vile hana akaunti za dola nje ya nchi wala mandege yanayorushwa nchini.

Hivi ni nani alimuambia Mheshimiwa Pinda kuwa tatizo la ufisadi nchini ni watu kuwa na akaunti nje ya nchi? Kama hilo ni kweli anasema nini kuhusu Chenge ambaye ana akaunti ya mamilioni huko Uingereza na bado ni Mbunge?

Nimeandika kwa kirefu juu ya hili na ninatumaini itakuwa kwenye mojawapo ya magazeti ninayoandika siku ya Jumatano. Maswali ambayo natafuta majibu yake: Ni kitu gani kitakufanya uridhike na kumsamehe Mkapa kwa kitendo chake? Je kurudisha Kiwira serikalini inatosha (kama vile aliyeiba ng'ombe akirudisha asishtakiwe kama wale wanaodaiwa kurudisha fedha za EPA?)

Je, sheria ifuate mkondo wake hata kama mhusika ni Rais mstaafu au tusiwaguse viongozi wetu wastaafu hata kama tunajua wamevunja sheria? Itakuwaje kama huko mbeleni tuje kusikie baadaye kuwa Rais fulani alipokuwa madarakani alimbaka mtumishi wake wa ndani, je tutamuachia kwa vile ni mstaafu?

NB: Ninafanya mambo kwa kibaba kutokana na hali ngumu ya uchumi kama mjuavyo japo kuna mambo mengi sana ya kufanya na kwa wale wanaojua mipango yetu KLHN kwa kweli sasa hivi tuko nyuma kwa karibu miezi mitatu. Tunaomba dua na sala zenu ili tuweze kufanikisha mipango yetu ili kuelekea 2010 mwamko mpya wa fikra uzidi kujikita miongoni mwa watu wetu.

460>_1191463
Ifuatayo ni taarifa ya habari ya saa mbili za Usiku Juni 10, 2009 kwenye TBC
[PLAY]
460>_1899457
Kwa usiku kucha kundi la wahuni waliojibatiza jina la "wanakijiji" na kutuchafua wengine walivamia eneo la Mhe. Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) na kuharibu mazao na kuchoma nyumba na kuiba mali mbalimbali, walifanya hivyo kwa kile ambacho gazeti la Mwananchi limeelezea kuwa "wanadai kwamba, kwa kuwa shamba hilo liko katika eneo lao wangepewa ili walitumie kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kujenga shule, hivyo kitendo cha serikali kuliuza kwa mtu wa nje ya kijiji hicho ni kunyanganya haki yao." Kitendo hiki ni cha aibu na kina fanana na vitendo vya uvamizi kule Zimbabwe au vile vilivyosababisha machafuko makubwa Kenya vya Mungiki. Ni vya kulaaniwa na kila mpenda haki na mwenye kuheshimu utawala wa Sheria. Ni kwa sababu hiyo tumepata nafasi ya kuzungumza na Bw. Kimaro jana kuhusu suala hili na kujaribu kutafuta maoni yake na kama kitendo hiki kitamfanya ahamishe uwekezaji huo wa Arumeru na kuupeleka sehemu nyingine kwani hawamtaki huko Arumeru! Sikiliza:
[PLAY]
460>_1896228
Siku ya Jumamosi nilialikwa kuwa mmoja wa wachangiaji katika kipindi cha "Tulonge Asubuhi" kinachorushwa na Star TV Jijini Mwanza. Mada kuu ilikuwa tulilojifunza kutokana na Uchaguzi mdogo wa Busanda. Wachangiaji wengine ambao nao walipata nafasi ya kuchangia kwenye onesho hilo la asubuhi ni pamoja na Erasto Tumbo (Chadema), na Amos Makalla (CCM) pamoja na wapiga simu wengine. Ni matumaini nitaendelea kupata nafasi kama hii ili kuendelea kuchochea mabadiliko ya kifikra ambayo mara zote hutangulia mabadiliko ya kura! Unaweza kuniandikia: mwanakijiji@mwanakijiji.com
[PLAY]
460>_1835385
Unaweza kusikiliza kwa kudownload kutoka hapa au kusikiliza moja kwa moja kwa kubonyeza "play" chini hapa.

http://www.box.net/shared/qfp38sfr3n

Ukisikiliza usiniulize, na wala usimwambie mtu mwingine. For your Ears Alone! M.M.
[PLAY]
460>_1810084
Ningeweza kukuambia kilichomo lakini sitakutendea haki; itabidi usikilize mwenyewe.
[PLAY]

Next Page