Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_1899457
Kwa usiku kucha kundi la wahuni waliojibatiza jina la "wanakijiji" na kutuchafua wengine walivamia eneo la Mhe. Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) na kuharibu mazao na kuchoma nyumba na kuiba mali mbalimbali, walifanya hivyo kwa kile ambacho gazeti la Mwananchi limeelezea kuwa "wanadai kwamba, kwa kuwa shamba hilo liko katika eneo lao wangepewa ili walitumie kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kujenga shule, hivyo kitendo cha serikali kuliuza kwa mtu wa nje ya kijiji hicho ni kunyanganya haki yao." Kitendo hiki ni cha aibu na kina fanana na vitendo vya uvamizi kule Zimbabwe au vile vilivyosababisha machafuko makubwa Kenya vya Mungiki. Ni vya kulaaniwa na kila mpenda haki na mwenye kuheshimu utawala wa Sheria. Ni kwa sababu hiyo tumepata nafasi ya kuzungumza na Bw. Kimaro jana kuhusu suala hili na kujaribu kutafuta maoni yake na kama kitendo hiki kitamfanya ahamishe uwekezaji huo wa Arumeru na kuupeleka sehemu nyingine kwani hawamtaki huko Arumeru! Sikiliza:
[PLAY]