June 07, 2009 09:43 PM PDT
Siku ya Jumamosi nilialikwa kuwa mmoja wa wachangiaji katika kipindi cha "Tulonge Asubuhi" kinachorushwa na Star TV Jijini Mwanza. Mada kuu ilikuwa tulilojifunza kutokana na Uchaguzi mdogo wa Busanda.
Wachangiaji wengine ambao nao walipata nafasi ya kuchangia kwenye onesho hilo la asubuhi ni pamoja na Erasto Tumbo (Chadema), na Amos Makalla (CCM) pamoja na wapiga simu wengine.
Ni matumaini nitaendelea kupata nafasi kama hii ili kuendelea kuchochea mabadiliko ya kifikra ambayo mara zote hutangulia mabadiliko ya kura!
Unaweza kuniandikia: mwanakijiji@mwanakijiji.com