Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_1750188
Salaam, Pamoja na habari mwanana za wiki hii ambazo zitagusa fikra zako na maoni ya kuthubutu ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote tunakuletea pia habari zinazoendelea kila wakati. Kwa kupata email ya habari mpya na kupokea kijarida chetu cha "Cheche" kwa kutumia barua pepe tuandikie kwenye anuani ya mhariri iliyoko kwenye kijarida. Kuna habari mbili kubwa ambazo zimeanza kusikika saa hii: a. Wakuu wa Mikoa wapanguliwa na kubadilishana vituo mbalimbali, hii inaonesha kugusa mikoa ya Tanga, Dar, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma n.k Kimsingi siyo habari kubwa inayostahili kwani kilichofanyika ni kubadilishana ofisi tu. Aliyeshindwa eneo moja kumpeleka jingine hakuondoi tatizo ambalo ni yeye! Baadhi ya mabadiliko hayo: Dr. Ishengoma toka Pwani kwenda Ruvuma Bi. Hajjat Amina Said toka Iringa kwenda Pwani Bw. Abdulazziz toka Tanga kwenda Iringa Bi. Monica Mbega toka Ruvuma kwenda Kilimanjaro (huyu ni yule Mkuu wa Mkoa wa "Kamtumbwi ka Kikwete") tunaendelea kufuatilia kujua wa Kilimanjaro ameenda wapi na kama Mbeya wamebadilishiwa (maana na siasa zao huko ni vurugu kuwa na Mkuu wa Mkoa ambaye ni mwenyeji wa huko!) b. Kuna habari kuwa ofisi za DECI zimefungwa au DECI yenyewe imesimamishwa. Utaona katika toleo letu la leo tulitoa wito huo kwani kuiacha kuendelea kufanya kazi katika mazingira ya sasa ni kulea uovu. Kwa hiyo tunasubiri tuone mwitikio utakuwaje kwani tangu makala zetu mbili (iliyotoka kwenye Cheche wiki iliyopita) na iliyotoka leo kwenye Mwanahalisi kuna watu wamechukizwa na wengine wameapa kufanya vitu vibaya endapo DECI itafungwa. Tunatumaini vikosi vyetu vya usalama viko tayari kusimamia haki. Na hii ni habari ndogo c. Kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya Ziwa, wiki hii wataanza kuona gazeti jipya la habari na maoni na tunarajia kuwa na makala za Mwanakijiji humo pia. Kaeni chonjo. Basi na sisi na twende na tuwe "Cheche"! Jipatie nakala ya cheche: http://www.forums.mwanakijiji.com/showthread.php?t=729