Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_1632441

Mpango wa serikali kutaka kuyanunua majenereta ya kuzalisha umeme ambayo yaliletwa nchini na Kampuni ya Dowans katika mkataba wake na kampuni feki iliyoumbuliwa ya Richmond hautokani na kulazimika kufanya hivyo bali hali halisi ya hali ya nishati nchini ndiyo inalazimisha serikali kupanga kuchukua hatua hiyo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja alipozungumza na tovuti hii hapo jana kuelezea kile ambacho kinaonekana mgongano wa kimtazamo kati ya Wizara, kamati mbili za Bunge na hisia za makundi ya Watanzania.

Akizungumza nasi kwa kirefu Mhe. Ngeleja amejenga hoja kuwa suala la ununuzi wa mitambo hiyo halihusiani na masuala ya kifisadi kama wengi wanavyohisi huku yeye mwenyewe akisema kuwa "siyo wote mafisadi". Bw. Ngeleja alitumua muda mrefu kushawishi kuwa mpango huu ni mzuri kwa maslahi ya Taifa na kuna kila sababu ya kuangalia kwa ukaribu na kuubali.

Ni kwa kiasi gani ameweza au anaweza kushawishi uamuzi ni wawasikilizaji wetu wenyewe. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kwenye tovuti yetu hii au kwa kusikiliza kupitia tovuti yetu ya http:/www.mwanakijiji.podomatic.com ambapo unaweza kuyapata mahojiano hayo kwenye Itunes au Ipod yako. Sikiliza wewe mwenyewe kama Mhe. Ngeleja amejenga hoja ya kukushawishi kukubali serikali inunue mtambo huu au ungependa serikali isiendelee nao.

Sisi katika tovuti yetu tutatoa msimamo wetu kwenye kijarida cha Cheche kitakachotoka hapo kesho.

[PLAY]