Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_1548349

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametumia nafasi yake ya kujibu maswali Bungeni kugusa hisia za wabunge kwa kuonesha uchungu uliomgusa kufuatia mauaji ya maalbino ambayo yamekuwa yakiendelea nchini.

WM Pinda alimwaga machozi hayo baada ya kuulizwa kuhusu kufafanua kauli yake iliyotaka watu watakaoshukiwa au kutuhumiwa mauaji ya albino na wao kuuawa hapo hapo. Alipoulizwa kwanini ahalalishe mauaji hayo na kwanini atoe kauli zinazonesha kukikanzina na utawala wa sheria na Katiba ambao ni msingi wa TAifa letu, Mhe. Pinda alielezea kwa kirefu juu ya safari yake na yale aliyoyaona na kuelezea kuwa mtu yeyote akiyaona aliyoyaona hana sababu tena ya kufuata sheria bali kuchukua hatua mikononi.

Alielezea kauli yake kuwa ni ya kutishia watuhumiwa hao kuwa wajue serikali iko fed up na mauaji ya Albino. Hata hivyo hakuifuta kauli hiyo wala kusema kwamba watuhumiwa wote wafikishwe kwenye vyombo vya sheria au kuwataka wananchi kuhakikisha katika kupambana na mauaji haya wao wenyewe hawajikuti wakivunja sheria za nchi.

Swali ambalo linaonekana kuwagawa wananchi ni je kutokana na mauaji haya ya albino ipo haja ya wananchi kufuata sheria au wakimkuta mtu wanayemdhania kuwa ndiye muhusika wamchukulie hatua mikononi kama inavyofanywa kwa vibaka, wezi wa kuku na watuhumiwa wengine ambao mara nyingi hupata kibano papo kwa hapo?

Msikilize Pinda akikwepa kujibu swali aliloulizwa.

[PLAY]