Karibu wiki moja iliyopita Mhe. Zitto Kabwe alizungumza na jumuiya ya Watanzania waishio Jimbo la Michigan nchini Marekani. Mazungumzo hayo yaliyofanyika wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyoandaliwa Bw. Zitto yaligusia mambo mbalimbali na hasa kuwataarifu wanajumuiya hiyo mambo mbalimbali yanayoendelea nyumbani na pia kusikiliza maoni na maswali yao.
Matangazo ya leo basi ni hotuba ya Mhe. Zitto kwa jumuiya hiyo na sehemu ya maswali na majibu, yote ni uncut and an edited. Makosa mengine yoyote ya kurekodi hasa mwanzoni kidogo ni ya KLHN.
Pichani Mhe. ZItto akijiandaa kuzungumza na wanajumuiya ya TAMI - Tanzanians Association of Michigan. Huko Detroit eneo la Maili Nane.


![[PLAY]](/img/play_button.gif)