Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
69183665
460>_900839

Gavana wa Benki Kuu, Dk Beno Ndullu (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB), Andulile Mwakalyelye (kulia) alipotembelea mabanda wakati wa mkutano wa Makandarasi na Taasisi za fedha kwenye viwanja vya Karimjee Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili wa Bodi ya Makandarasi, Mhandisi Boniface Muhegi

Kuna mahali katika serikali yetu watu hawawasiliani. Nina kila sababu ya kuamini kuwa kuna mtu ambaye hafikishi habari kwa mwingine kiasi kwamba tumefikia mahali watumishi wa wizara ile ile na ambao kimsingi wanatakiwa kuwasiliana inaonekana hawawasiliani.

Hebu fikiria, Katibu Mkuu wa Hazina anasimama na kutetea maamuzi yake kuwa alipotia sahihi kwenye kampuni ya Tangold kama mmoja wa wakurugenzi alijua kuwa kampuni hiyo ni mali ya serikali. Siyo hivyo tu aliyekuwa Waziri wa Fedha Bi. Zakhia Meghji aliliambia Bunge kuwa kampuni hiyo iliyochukua nafasi ya kampuni nyingine ya "serikali" ya Meremeta ni mali ya serikali.

Kabla hilo halijatulia Gavana wa Benki Kuu ambayo kampuni hiyo ilimegewa karibu Bilioni 155 kwa vile ni kampuni ya serikali anaibuka kesho yake na kusema kuwa watu wasiihusishe Benki hiyo Kuu na Kampuni hiyo kwani hakuna ushahidi wowote kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na serikali

Sasa nani anaweza kuwa na uwezo wa kujua juu ya Kampuni hii kati ya Katibu Mkuu Hazina ambaye ni Mkurugenzi wa Tangold na Gavana wa Benki Kuu iliyotoa mabilioni kwa taasisi hiyo?

Hivi Watanzania tumekosa nini hadi tuburuzwe kama watoto wanaochezewa mchezo wa Karata tatu? Hivi mtu akimuuliza Kikwete kama Kampuni ya Tangold ni ya serikali atakuwa na jibu kweli wakati Hazina na Benki Kuu hawakubaliani?

Hili nalo linanikumbusha juu ya Mgodi wa Buhemba ambao tuliambiwa kuwa ni mali ya serikali lakini Mkaguzi Mkuu wa serikali anasema hana jina hilo katika orodha ya makampuni ya serikali. Sasa mgodi huo unalindwa na Polisi, nani anaumiliki?

Kuna mtu yeyote anaweza kutoa jibu? Hivi kweli tumefikia mahali hatujui hata nani anamiliki mgodi mkubwa kama Buhemba? Hivi tukiuliza nani anamiliki Ikulu yetu tunaweza kuwa tunatafuta ugomvi? Tukisema kuna mafisadi hivi kweli watakuwa na sababu ya kututafuta? Au tuanze kampeni kwa kupitia wahisani dhidi ya misaada au tutaambiwa tunataka watu wa kawaida wapate shida? Ni nini kitatufanya tuchore mstari?

Naomba nitoe wito kwa Waziri wetu wa Fedha atuambie bila kujiuma uma, ni nani anamiliki Tangold na Buhemba? is this too much to ask as citizens of our beloved country au ndio imekuwa ni mradi wa Usalama wa Taifa?