Hadi gazeti la Guardian litutangazie kuwa Waziri wetu ameficha Bilioni kisiwani Jersey (thanks Yebox2) wao kina RO walikuwa wapi?
Hadi Kamati Teule ilipotuambia rasmi kuwa RDC ni kampuni hewa RO na timu yake walikuwa wapi?
Niendelee kuorodhesha ushahidi wa uzembe uliokithiri na uvivu wa kufikiri wa taasisi nyeti ya Usalama wa Taifa? Kama wameshindwa kugundua matukio ya economic sabotage yanayoendelea nchini wana faida gani? Hii ya kusafiri na Rais na kutumia vi ear pieces na makoti marefu kama vile wao Secret Service?
Kwanini basi Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Rashid Othman (Pichani) asijiuzulu kwa ajili ya Usalama wa Taifa!!!
Lakini kabla yake Bw. Cornel Apson Mwang'onda na yeye alishikiri vipi katika kuzembea kulilinda Taifa letu na ni nani mwenye ujasiri wa kumuita na kumhoji?
Isije kuwa Usalama wa haki ya kula na kutanua na fedha za walipa kodi wa Tanzania lakini inapokuja katika kuelezea walifanya nini na pesa hizo inakuwa mbinde?
yes I said it!

