Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
powered by podOmatic
460>_718540
Wakiwa madarakani Rais Benjamini Mkapa na Waziri wake wa Nishati na Madini waliingia ubia na kuanzisha kampuni ya Tanpower Resources. Wakati Yona analiambia Bunge kuwa wanatafuta wawekezaji wa "kufufua" Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, sirini walikuwa wanapanga yeye na Rais wake kuwa "wawekezaji" hao watakuwa ni wao wawili. Na miezi michache kabla Rais Mkapa hajaachia madaraka, Mgodi wa Kiwira ulikuwa chini ya viongozi hao wawili wakiwa na hisa zaidi ya asilimia 80. Hadi leo hii hakuna aliye tayari kueleza ni jinsi gani viongozi hao wawili waliweza kusimamia uuzwaji wa Kiwira wakati wao wenyewe wakiwa ndio wanunuzi wakubwa. Kabla watu hawajashangaa maajabu hayo ya "Musa" wakajikuta wanashuhudia serikali ya awamu ya nne ikiingiza Tanesco kwenye mkataba na kampuni ya kina Mkapa na Yona ambao waweza kuligharimu taifa zaidi ya shilingi bilioni 300. Binafsi naona inatosha kuoneana aibu; Rais Mkapa na Yona Wanyang'anywe mgodi huo ambao walijipatia kwa kutumia madaraka yao vibaya.

Tatizo ni kuwa nani, atamfunga paka kengele?

[PLAY]