November 17, 2007 07:25 AM PST
Leo kama mnavyofahamu kulikuwa na makongamano ya wanafunzi jijini Dar-es-Salaam. Moja lilifanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuhutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Pius Msekwa na lile jingine lililofanyika Ukumbi wa DDC na kuhutubiwa na wasomi mbalimbali na viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo Mhe. Zitto Kabwe. Nilipata nafasi ya kutuma salamu za mshikamano kwa kongamano la DDC baada ya kuombwa kutuma ujumbe huko. Walioko nyumbani waliupata kwa njia ya maandishi, lakini hapa unaweza kuupata kwa kusikia.
Ujumbe wangu unaitwa: "Wasomi waongoze mapambano ya Kifikra".
M. M.